Shirika la Upelelezi Nchini Marekani (FBI) limetoa wito kwa Bunge la Congress na Ikulu ya White House kuipatia pesa kwa haraka idara hiyo, huku ikitahadharisha kuwa upungufu wa pesa za matumzi umeanza kuathiri shughuli za FBI.
Wafanyakazi wa FBI kwa mara ya kwanza Ijumaa hii hawakupata mishahara yao, wakati leo ikiwa ni siku ya 20 baadhi ya idara za serikali kuu zikiwa zimefungwa kutokana na mvutano kati ya Rais Donald Trump na Wademocrats juu ya ujenzi wa ukuta kwenye eneo la mpaka kati ya Marekani na Mexico.
“Hali imekuwa mbaya sana, kazi muhimu inayofanywa na FBI inahitaji pesa,” umesema umoja huo unaowakilisha wafanyakazi elfum13, katika malalamiko waliyo wasilisha jana kwenye bunge na white House.
Hata hivyo, tangu shughuli ya baadhi ya idara za serekali kuu kufungwa hapo Disemba 22, baadhi ya wafanyakazi laki 8 wa serikali kuu walilazimika kukaa nyumbani, wengine waliendelea kufanya kazi bila kulipwa mishahara, miongoni mwa hao kuna wafanyakazi elfu 5 wa FBI.