Klabu ya Barcelona imethibitisha kuwa haitocheza Camp Nou wakati wa msimu wa 2023-2024, kufautia Uwanja huo kuwa kwenye mpango wa kufanyiwa ukarabati.
Rais wa Barca Joan Laporta na Halmashauri ya Jiji la Barcelona wamekubaliana kuwa klabu hiyo itahamia Lluis Companys Olympic Stadium (Montjuic) ambapo michezo yao yote za nyumbani itafanyikia.
Uwanja huo wa muda una uwezo wa kuchukua mashabiki 55,000 walioketi, na utatumika kwa msimu mmoja.
Ukarabati wa uwanja mkongwe wa Barcelona ambao utaanza mwezi huu unakadiriwa kugharimu Pauni Bilioni 1.2. Klabu hiyo itaendelea kutumia sehemu kadhaa za uwanja huo hadi mwakani.