Barcelona imefungua kesi Mahakamani kupinga usajili wa Lionel Messi kujiunga na PSG, wakidai klabu hiyo haiwezi kumsajili mchezaji huyo kutokana na rekodi mbaya ya mapata na matumizi ya klabu hiyo, ambapo wanaamini wakifanya hivyo watavunja kanuni ya Financial Fair Play.

Mawakili wa Barcelona wamewasilisha malalamiko kwenye Mahakama ya Rufaa barani ulaya wakitaka PSG izuiliwe kufanya usajili wa Lionel Messi kutokana na takwimu za kiuchumi, kwa sasa Messi ni mchezaji huru na imeripotiwa kuwa mchezaji huyo bora wa Dunia mara 6 yupo kwenye hatua za mwisho za kujiunga na PSG.

Kwa mujibu wa malalamiko yaliyowasilishwa na Barcelona yanadai kwamba hali ya matumizi ya pesa ya PSG ni mabaya zaidi ukilinganisha na klabu yao, hivyo wanaamini PSG hawatahili kumsajili Messi kwa sababu watavunja kanuni ya (Financial fair Play) kanuni hii inavitaka vilabu barani ulaya vitumie pesa kulingana na kiwango cha pesa halali walizoingiza kutokana na shughuli za mpira.

Ripoti za mishahara ya PSG kwa msimu wa 2019-20 zinaonyesha kuwa wastani wa mishara ya wachezaji wa klabu hiyo ilikuwa imefikia asilimia 99% wakati FC Barcelona wastani wao ulikuwa ni asilimia 54 % na sasa inaaminika endapo kama PSG wakimsajili Messi basi watakuwa wamevunja kannuni hiyo kwani matumizi yao yatakuwa yamezidi kipato chao.

Barcelona wameshindwa kumpa La Purga mkataba mpya kwa sababu ya kanuni hiyo ya Finacial Fair Play, inaonyesha endapo kama mchezaji huyo angesaini mkataba mpya basi kiwango cha matumizi kwenye mshahara kingefika asilimia 110% na wangekuwa wamevunja kanuni hiyo kitu ambacho ni kinyume na kanuni za mapato na matumizi kwa vilabu barani ulaya.

Kamwaga: Tumepokea ofa kutoka Kaskazini
Ni uongo, Tuisila hajasajiliwa RS Berneke