Meneja wa klabu bingwa nchini Hispania FC Barcelona, Luis Enrique amesema ana matarajio makubwa ya kuketi chini ya mshambuliaji wa klabu hiyo Pedro na kupanga mikakati mipya ambayo itamzuia kuondoka katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Hispania, amekua katika mawindo makali ya Man Utd kwa kipindi cha majuma kadhaa na taarifa zilidai kwamba ataruhusiwa kuelekea nchini England mara baada ya mchezo wa Uefa Super Cup unaochezwa hii leo mjini Tbilisi nchini Georgia, ambapo FC Barcelona watapapatuana na Sevilla.

Enrique, amesema ana uhakika wa kumaliza matatizo yaliyojitokeza kati yake na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28.

Imeelezwa kwamba wawili hao walipisha mitazamo kutokana na falsafa za uchezaji wa FC Barcelona ambapo tangu alipoingia Enrique klabuni hapo, amekua akitumia mfumo unaomnyima nafasi Pedro ya kucheza kila mwishoni mwa juma na badala yake hutoa fursa kwa Messi, Suarez pamoja na Neymar.

Enrique amesema mbali na kumpigania Pedro asiondoke, pia atasimama kidete ili kuhakikisha kila aliopo kikosini mwake kwa sasa aendelee kubaki kwa lengo la kusaka mafanikio zaidi ya yale waliyoyafikia msimu uliopita.

FC Barcelona Kidume Uefa Super Cup
Real Madrid Kumrudisha Cheryshev