Mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona wameingilia kati na kuvuruga mpango ya wapinzani wao Real Madrid wa kumsajili kiungo kutoka nchini Ureno na klabu ya Valencia, Andre Gomes.

Gazeti la Mundo Deportivo la nchini Hispania limeripoti kwamba FC Barcelona wameingia kwa kasi katika harakati za kuvuruga mpango ya Real Madrid, na kufikia hatua ya kukubali ada ya usajili wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22.
Gazeti hilo limeendelea kueleza kuwa, Gomez atasaini mkataba wa miaka mitano mara baada ya kufanyiwa vipimo vya afya mwishoni mwa juma hili.
Usajili wa kiungo huyo unatajwa kama mbadala wa Arda Turan ambaye tayari ameshawekwa sokoni katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.
Hata hivyo mapema hii leo, FC Barcelona wamethibitisha taarifa za kukubali ada ya uhamisho wa kiungo huyo na kuziandika katika ukurasa wao wa mtandao wa Twitter.


Gomes, alikuwa sehemu ya kikois cha timu ya taifa ya Ureno kilichotwaa ubingwa wa Euro 2016 baada ya kuichapa Ufaransa bao moja kwa sifuri, katika mchezo wa hatua ya fainali uliochezwa Julai 10 mwaka huu mjini Paris.
Mbali na Real Madrid kuvurugiwa mpango ya usajili wa mchezaji huyo, pia klabu ya Chelsea itakua imethirika kutokana na jina la Gomez kuwa sehemu ya wachezaji ambao walitarajiwa kusajiliwa na meneja wao mpya Antonio Conte.

Alipwa kubikiri wasichana, wazazi wamkabidhi watoto wao na kufanya sherehe
Roberto Mancini Aguswa Na Mkasa Wa Mario Balotelli