Mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona, wamekubali kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Sevilla CF, Kevin Gameiro.

Barcelona wamefikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji huyo, ambaye anatarajiwa kuwa mchezaji wanne kusajiliwa na meneja Luis Enrique katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

Makubaliano kati ya pande hizo mbili, yalifikia tamati mwishoni mwa juma lililopita na kuanzia hii leo, Gameiro anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya yake kabla ya kukamilisha taratibu zote za uhamisho.

Taarifa za awali zinadai kwamba FC Barcelona wamekubali kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29, kwa ada ya Euro milion 40.

Wachezaji wengine ambao tayari wameshakamilisha usajili wa kujiunga na FC Barcelona kwa ajili ya msimu wa 2016/17 ni Samuel Umtiti (Olympique Lyonnais), Lucas Digne (Paris Saint-Germain FC) na Andre Gomes (Valencia CF).

Hakuna Kanuni za kukagua Wimbo Kabla ya Kuachiwa- Roma
Per Mertesacker: Ushindani Utakua Mkubwa Msimu 2016/17