Kocha Mkuu wa FC Barcelona Xavi Hernández amekanusha taarifa za Kiungo kutoka nchini Ujerumani Ilkay Gündogan zinazodai yupo njiani kuikacha timu hiyo na kuelekea Saudi Arabia.

Xavi ameeleza hayo alipozungumza na vyombo vya habari kuwa mchezaji huyo ataendelea kuwepo ndani ya FC Barcelona hadi mwishoni mwa msimu wa 2023/2024.

Kocha huyo alifafanua kuwa hii si mara ya kwanza kwa Gündogan kuhusishwa kutaka kủondoka klabuni hapo, kwani anaamini huo ni mpango wa kutaka kuvuruga mambo ndani ya klabu hiyo.

“Nimepata habari Gündogan anaenda kucheza soka Saudi Arabia hili halipo ni uzushi tu,”

“Amewahi kuhusishwa kwenda Real Madrid, najua kuna wakati alikuwa hana furaha ndani ya Barca lakini huo ni uzushi kwamba anaenda Saudi Arabia,”‘ amesisitiza kocha huyo.

Kauli hiyo, imekuja baada ya gazeti la Asharg To the-Awsat kueleza kuwa mchezaji huyo wa Ujerumani amefungua mlango wa mazungumzo na klabu za Saudi Arabia.

Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Saudi Arabia Saad To the-Ladhim amethibitisha kuwa mchezaji huyo huenda akatua nchini Saudi Arabia.

Habari zaidi zinaeleza kuwa mchezaji huyo huenda akatua ndani ya timu moja wapo kati ya Al Nassr au Al Ittihad.

Nyuki watajwa ajali Basi Lindi
Acheni mazoea, fuateni sheria: Madereva waonywa