Mabingwa wa Soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich wametuma ofa ya pili yenye thamani ya Euro milioni 80 kwa mshambuliaji, Harry Kane, ingawa Tottenham Hotspur bado imesisitiza kuwa haina nia ya kufanya mazungumzo.
Nahodha huyo wa England amebakiza mwaka mmoja tu kwe- nye mikataba wake wa sasa.
Spurs wamekuwa na uhakika wa kumbakisha Kane kwa muda mrefu ujao na tayari wamekataa ofa ya kwanza ya euro milioni 70 kutoka kwa mabingwa hao wa Ujerumani Bayern mapema msimu huu wa majira ya joto.
Tottenham hawana mpango wa kumuuza mchezaji huyo na 90minutes inaelewa kuwa hakuna bei inayoweza kuamuliwa na uongozi wa klabu huku Bayern na kocha Thomas Tuchel wakishinikiza makubaliano.
Kocha wa zamani wa Chelsea, Tuchel anataka Kane aongoze safu hiyo ya ushambuliaji na ana matumaini ya kupata dili katika miezi ijayo.
Hata hivyo, Spurs wanabakia kuimarika na hawana nia ya kumruhusu mfungaji huyo bora wa pili katika historia ya Ligi Kuu England kuondoka.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, alikuwa katika kiwango kizuri tena 2022/23, akifunga mabao 30 huku timu yake ikimaliza nafasi ya nane.
Klabu kubwa za Ulaya zimeonesha nia ya kumtaka mchezaji huyo zikiwamo Manchester United, Paris Saint-Germain na Real Madrid.
Kocha mpya Ange Postecoglou atatumaini Kane bado ataendelea katika klabu hiyo msimu wa 2023/24 utakapoanza.
Spurs wamemwongeza Dejan Kulusevki kwenye safu yao ya ushambuliaji huku pia Guglielmo Vicario na James Maddison wakitua hapo.