Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (StarTimes League) inaendelea wikiendi hii kwa michezo 12 kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini ikiwa katika mzunguko wa kumi, huku kila timu ikisaka pointi tatu muhimu kuweza kupanda Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao wa 2016/2017.

Kundi A, Jumamosi Mji Mkuu watawakaribisha Ashanti United uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Kiluvya United dhidi ya Polisi Dar uwanja wa Mabatini – Mlandizi, Africa Lyon v Friends Rangers uwanja wa Karume jijini Dar es salaam huku Polisi Dodoma wakiwa wenyeji wa KMC FC uwanja wa Mgambo Mpwapwa.

Kundi B, Polisi Morogoro watacheza dhidi ya Lipuli uwanja wa Jamhuri Morogoro, JKT Mlale watawakaribisha Kimondo FC uwanja wa Majimaji mjini Songea, Kurugenzi FC dhidi ya Ruvu Shooting uwanja wa Wambi Mafinga na Njombe Mji watakua wenyeji wa Burkinafaso uwanja wa Amani- Njombe.

Kundi C, Panone FC watawakaribsha maafane wa JKT Kanembwa uwanja wa Ushirika mjini Moshi, Polisi Mara watacheza dhidi ya JKT Oljoro uwanja wa Karume mjini Musoma, Rhino Rangers dhidi ya Geita Gold uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora, huku Mbao FC wakicheza dhidi ya Polisi Tabora mchezo utakaonyeshwa moja moja na kituo cha Star TV.

Benitez Ajipaka Mafuta Kwa Mgongo Wa Chupa
Man Utd Wafikiria Kumrejesha Nyumbani Adnan Januzaj