Bingwa mtetezi wa Wimbledon Roger Federer amemshinda mchezaji namba moja kwa ubora duniani Rafael Nadal kwa seti 6-4 6-3 katika michuano ya Shanghai Master.

Federer ambaye amepoteza michezo minne tu kwa mwaka 2017, alikuwa katika kiwango cha juu na kushinda ndani ya dakika 72.

Ushindi huo unamfanya Roger Federer kuwa na vikombe sita mwaka huu katika michuano tofauti ukiwa pia ni ushindi wake wa nne kwa mwaka huu dhidi ya Nadal.

Mchezaji huyo ameshinda mataji 94 katika maisha yake ya uchezaji tenisi huku 19 ikiwa ni grand slam. Federer amefikia rekodi ya Ivan Lendl lakini wote wanapitwa na Jimmy Connors wa Marekani mwenye vikombe 109.

Video: Sababu za usalama zamkwamisha Lowassa, Wahamiaji haramu sasa pasua kichwa
Nyumba za ibada zakumbwa na bomoabomoa leo