Uongozi wa Klabu ya Liverpool wamepanga kutumia pesa watakayoipata kwenye dili la kumuuza kiungo Fabinho katika dirisha hili ili kumsajili kiungo wa Fulham, Joao Palhinha.

Liverpool inatarajiwa kupokea walau Pauni 40 milioni kwenye dili la kumuuza Fabinho kwenda Al-Ittihad ya Saudi Arabia na Palhinha anaonekana kuwa mbadala wake huko Anfield.

Licha ya ukweli kwamba Palhinha anauzwa zitatakiwa zaidi ya Pauni 50 milioni ili kuipata saini yake kwani West Ham United ambayo kwa sasa ndio ipo kwenye harakati za kutaka kumsajili imeshawasilisha ofa ya Pauni 45 milioni, lakini imekataliwa na mabosi wa Fulham.

West Ham United inapambana kuhakikisha kwamba inanasa kiungo kutokana na kuondokewa na nahodha na mchezaji wake tegemeo katika eneo hilo, Declan Rice kwenye dirisha hili.

Fabinho

Pamoja na timu hizo kunyemelea saini ya mchezaji huyu pia kuna timu kibao kutoka katika ligi kubwa tano za Ulaya ambazo ama zimashaulizia juu ya bei au zimeonyesha nia ya moja kwa moja kutaka kumsajili.

Pamoja na hayo, mchezaji huyu ameonyesha nia ya kuondoka katika kikosi hicho kwenda kutafuta changamoto nyingine katika timu zingine.

Supastaa huyu wa kimataifa wa Brazil ni miongoni mwa mastaa walioonyesha viwango bora kwenye Ligi Kuu England katika msimu uliopita ambapo alicheza mechi 40 za michuano yote. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.

40 ya Matapeli ILE PESA TUMA HUMU imewakutia Tanga
Afisa wa Polisi akamatwa na misokoto 40 ya Bangi