Ikiwa itafanikiwa kumuuza Kylian Mbappe kwenda Saudi Arabia, Klabu ya PSG itatumia kiasi hicho cha pesa kulipa Pauni 100 milioni na kumsajili Mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane katika dirisha hili, licha ya ukweli kwamba akili ya Kane inafikiria kujiunga na Mabingwa wa Ujerumani FC Bayern Munich pekee.

PSG wamekuwa wakitajwa kutaka kumsajili Kane tangu dirisha hili lilipoanza lakini kuna wakati iliachana na mpango huo kutokana na kiasi kikubwa cha Pesa kinachohitajika na Spurs ili kumpata mkali huyo wa mabao wa kimataifa wa England.

PSG itawahitaji kuweka ofa nono zaidi na kuharakisha mchakato kwani ripoti zinadai Kane yupo kwenye harakati za kutafuta nyumba jijini Munich.

Mbali ya Kane, taarifa zinadai kwamba PSG huenda ikatumia pesa hiyo pia kumsajili Mshambuliaji wa SSC Napoli, Victor Osimhen kama mbadala wa staa huyu.

Kane ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu ujao 2023/24, anataka kuondoka Spurs kwa ajili ya kuchezea timu itakayompa nafasi ya kushinda mataji.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 27, 2023
Novak Djokovic aivuruga Canada