Watalamu wa Afya nchini wametakiwa kusimamia fedha zinazotolewa na wadau wa maendeleo, ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Wananchi kama ilivyo azma ya Serikali.
Wito huo umetolewa Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel wakati akifunga kikao kazi cha tathmini ya namna Tanzania ilivyoweza kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Uviko-19.
Amesema, “zinakuja fedha nyingi kutoka kwa wadau, lakini tukishuka chini katika ngazi ya msingi hatuoni matokeo chanya, tuige mfano wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan namna alivyotumia fedha za Uviko katika kuboresha huduma za afya.”
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Dharura na Maafa Wizara ya Afya, Dkt. Angela Samwel amesema mapendekezo yote yaliyotolewa na watalaamu pamoja na wadau walioshiriki kwenye tathmini hiyo yatafanyiwa kazi.