Mamia ya Wananchama wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo – FEMATA, kutoka mikoa mbalimbali Nchini, wamekutana jijini Dodoma kujadili mambo mbalimbali, ikiwemo usuluhishi wa migogoro inayotokea baina yao pamoja na kuendelea kufanya kazi kwa umoja.

Kikao hicho, kilichoanza mwanzoni mwa juma hili kilifungwa na Kamishana wa Madini, Dkt. Abdulrahman Mwanga, aliyemuwakilisha Waziri wa Madini, Antony Mavunde na kusema kwa sasa wachimbaji wanaona fahari kutokana na sekta hiyo kuwa na watu walioamua kufanya kazi na kuleta mabadiliko chanya.

Mbali na washiriki, kikao hicho pia kilitoa fursa kwa baadhi ya wadau kutoa elimu kwa wachimbaji kuhusu faida ya kujiunga na bima mbalimbali.

Kikao hicho kinajiri siku moja kabla ya kufanyika kwa hafla ya uzinduzi wa mitambo ya uchoraji kwa ajili ya wachimbaji wadogo wa madini pamoja na mitambo ya STAMICO, jijini Dodoma.

Habari Kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 22, 2023
Luis Suarez kumalizia soka lake Marekani