Rapa Fetty Wap amekamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na genge la wauzaji wa Dawa za kulevya.

Fetty Wap, 30, ambaye jina lake halisi ni Willie Junior Maxwell II, alikana hatia na kuamriwa azuiliwe bila dhamana kwenye kesi inayomkabili siku ya Ijumaa, The Associated Press iliripoti.

Kwa mujibu wa  afisa wa kutekeleza sheria, msanii huyo alikamatwa katika uwanja wa Citi Field huko Queens, ambapo  tamasha la muziki la Rolling Loud lilifanyika siku ya Alhamisi Oktoba 28, 2021.

Dawa hizo zilidaiwa kusambazwa kwa wafanyabiashara walioziuza huko Long Island na New Jersey.


“Tutaendelea kufanya kazi bila kukoma na washirika wetu wa utekelezaji wa sheria ili kuweka vitongoji vyetu salama kutokana na janga la dawa hatari za kulevya na vurugu za bunduki.”

Hati za upelelezi uliofanyika wakati wa uchunguzi zilipata takriban dola milioni 1.5 taslimu, kilo 16 za kokeini, kilo mbili za heroini, tembe nyingi za fentanyl, bastola mbili, bunduki, na risasi kadhaa.

Kwa nujibu wa sheria za nchini Marekani, Iwapo Fetty Wap na washtakiwa wote watakutwa na hatia,  watakabiliwa na hukumu ya hadi kifungo cha maisha jela.

Navarro Gray, wakili wa Fetty Wap, alisema “Tunaomba kwamba hii yote iwe ni kutoelewana sawa sawa tukitumai ataachiliwa ili tuweze kusuluhisha mambo haraka.”

Fetty Wap awali alikamatwa mwaka wa 2019 kwa makosa matatu ya betri, na mwaka wa 2017 kwa malipo ya DUI baada ya polisi kusema alinaswa akiendesha gari kinyume cha taratibu za sheria, barabara kuu ya New York City.

Rapa huyo anafahamika zaidi kwa wimbo wake wa “Trap Queen,” uliofanikiwa kufanya vizuri sana mwaka 2014, ambao ulifika nambari 2 kwenye chati za Billboard Hot 100.

Mkakati wa kuendeleza sekta ya mifugo na Uvuvi wawasilishwa
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 30, 2021