Msanii Fid Q amesema hana mpango wa kuingia kwenye siasa licha ya kupokea ushauri kutoka kwa mashabiki wake.

Mkali hiyo kutoka Mwanza amesema amekuwa akipokea ujumbe kutoka kwa watu mbalimbali wanaofutilia kazi zake, wengi wakimshauri awanie nafasi ya ubunge.

Akizungumza na Bongo.Home ya Times fm, Ngosha amesema haoni ulazima wa kuingia kwenye siasa kwa kuwa mchango anaoutoa kwenye jamii kupitia muziki ni mkubwa kuliko atakaoutoa akiwa bungeni.

“Nimekuwa nikipokea comment nyingi kwamba Fid vipi upande huo, ubunge unaweza kukufaa. Lakini mimi ninawaambia waniunge mkono kwenye muziki naweza badilisha jamii yangu kuliko kwenye siasa na nahisi nikiingia bungeni nitakuwa muoga,” amesema Fid Q.

Miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia wasanii wengi wakiingia kwenye siasa na kuwania ngazi tofauti za uongozi, miongoni mwao ni Joseph ‘Profesa Jay’ Haule mbunge wa Mikumi (Chadema) na Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi, Mbunge wa Mbeya mjini (Chadema).

Mbowe kuzungumzia afya ya Lissu, michango
Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 17, 2017