Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi -WCF, umeendelea kuboresha na kuhakikisha inafikisha huduma muhimu kwa wadau nchi nzima kwa njia ya mtandao, ili kufanikisha malengo kusudiwa.
Hayo, yamebaishwa hii leo Machi 2, 2023 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa WCF Dkt. John Mduma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mfuko huo na kusema hadi kufikia Juni 30 2022 walikusanya Shillingi 241.48 Bilioni ikiwa za mapato ya uwekezaji.
Amesema, huduma hizo za kimtandao ni pamoja na usajili wa mwananachama, Wanachama wa Mfuko ambao ni Waajiri, kupata cheti cha Usajili, kuwasilisha michango kila mwezi ambapo mfuko hupokea mchango kupitia nambari ya udhibiti inayopatikana kwa njia ya Mtandao.
“Hadi kufikia tarehe 30 June 2022,Mfuko umekusanya jumla ya Shillingi Billioni 241.48 toka kwenye mapato yanayotokana na uwekezaji” Amesema Dkt. Mduma.
Aidha, ameongeza kuwa kabla ya kuanzishwa kwa WCF malipo ya fidia nchini kwa mwaka mzima yalikuwa chini ya Shillingi millioni 200 lakini baada ya kuanzishwa kwa Mfuko huo malipo yanaongezeka kila mwaka.
“Mfuko huu umekuwa na faida kubwa kwani lengo,lake kubwa ni kuwakomboa wafnykazi waliopata madhili ama majanga wakiwa kazini kutoka katika dimbwi la umasikini ambapo takwimu za hivi karibuni zikionesha tangu kuanzishwa, idadi ya wanufaika wa Mfuko imefikia 10,454 ambao wamelipwa jumla ya shilingi Billioni 49.44,”amesema Dkt.Mduma.
Katika hatua nyingine, Dkt.Mduma amesema kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Machi 2021 hadi Februari 2023 Waajiri wapya 5,250 wamejisajili WCF huku kati ya waajiri hao asilimia 99.27% ni waajiri wakubwa ,huku asilimia 98.71% ni waajiri wa kati na waajiri wa chini ni asilimia 88.56%.