Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezielekeza Halmashauri zote nchini kuhakikisha maeneo yote yanayotwaliwa kutoka kwa wananchi yanalipiwa fidia kwa wakati, ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza siku za usoni.

Waziri Mkuu ametoa maelekezo hayo wakati akitoa hoja ya kuahirisha Mkutano wa 11 wa Bunge jijini Dodoma na kusema yapo malalamiko ya baadhi ya wananchi wa maeneo mbalimbali wakiwemo wa jiji la Dodoma kutolipwa fidia baada ya maeneo yao kutwaliwa na halmashauri ya jiji.

Amesema, “mahitaji ya uendelezaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwemo kuanzisha makazi yameendelea kuongezeka. “Ongezeko hilo ni muhimu likazingatiwa katika upangaji wa miji yetu hapa nchini.”

Aidha, Waziri Mkuu pia amezielekeza Halmashauri zote kupima maeneo kwa ajili ya shughuli za kiuchumi na kijamii, ikiwemo viwanja kwa ajili ya makazi badala ya kuacha wananchi kujenga kiholela.

Rada za Man Utd zamsoma Frenkie de Jong
TPBRC yawachimba mkara Mapromota