Shirikisho la soka duniani (FIFA) limetangaza kuifungia nchi ya Mali kushiriki michuano ya kimataifa, kwa madai ya serikali ya nchi hiyo kuingilia masuala ya soka.

Waziri wa Michezo wa Mali, Housseini Amion Guindo aliamua kuunda kamati ya muda kuendesha Shirikisho la Soka la Mali (FEMAFOOT) baada ya kuona uongozi uliokuwa madarakani haukua sahihi kwa mtazamo wa Serikali.

Lakini baada ya FEMAFOOT kufikisha malalamiko yake FIFA, shirikisho hilo la soka duniani, limeamuru serikali ya Mali, kuvunja kamati hiyo hadi Ijumaa (leo).

Baada ya kuona hakukuwa na utekelezaji hadi mishale wa saa tano na dakika hamsini na tisa (5:59) usiku, FIFA ilitangaza kuifungia Mali.

BARUA YA FIFA KWENDA FEMAFOOT
Katibu Mkuu wa FIFA, Fatma Samoura alisisitiza serikali ya Mali kuacha kuingilia michezo na kutaka Rais wa FEMAFOOT, Boubacar Baba Diarra aachwe aendelee kuongoza.

Fatma Samoura ndiye aliyeandika barua hiyo ya kuifungia Mali kushiriki michuano iliyo chini ya FIFA, jambo ambalo bila shaka ni pigo kwa Mali.

Felipe Monteiro Kutua Santiago Bernabéu Stadium
Video: Lissu apiga hodi jela, Bulembo afichua sh400 mil. alizopewa na Lowassa