Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba SC wamepewa muda wa kukamilisha malipo ya mchezaji wao wa zamani, Asante Kwasi ambaye alipeleka malalamiko yake Shirikisho la Soka Duniani ‘FIFA’ ili kupata stahiki zake.

Kwa mujibu wa barua ambayo waliandikiwa Simba kutoka chama cha wachezaji wa soka nchini Ghana ‘GPFA’ liliwaeleza kuwa wanapaswa kumlipa mchezaji huyo stahiki zake baada ya kushinda rufaa.

Barua hiyo iliandikwa Februari 26, 2020 zama za Mtendaji Mkuu, Senzo Mbatha ambaye kwa sasa ni Mshauri wa Kuelekea kwenye Mabadiliko ndani ya Young Africans.

Maamuzi ya FIFA yalifanyika awali Januari 15, 2020 na pia shauri la pili likatolewa maamuzi Februri 2020 baada ya mchezaji huyo kukata rufaa.

FIFA iliwaambia Simba SC kwamba wanapaswa kulipa kiasi cha doa za Marekani ‘USD’ 4,000 kwa ajili ya malipo ya stahiki za mchezaji Kwasi ambaye alisajiliwa na klabu hiyo akitokea Lipuli FC.

Habari zimeeleza kuwa Simba SC wamepewa muda kukamilisha malipo ya mchezaji huyo ambaye msimu wa 2017 alicheza Lipuli akitokea Klabu ya Mbao na aliachwa Simba msimu wa 2019.

Habari kutoka uongozi wa SimbaSC zimeeleza kuwa bado hawajapata taarifa hiyo.

TMA yatahadharisha Kimbunga Jobo kupiga Tanzania
Mahakama Marekani yamkuta Chauvin na hatia