Kikosi cha Coastal Union kimeanza maandalizi kwa ajili ya mechi ijayo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Tabora United, huku kocha msaidizi wa timu hiyo, Fikiri Elias akisema licha ya ugumu atarejesha heshima baada ya kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Simba SC kuwaamsha usingizini.
Wagosi walifumuliwa kwenye mechi iliyopigwa Alhamisi (Septemba 21) katika Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam na sasa wamerejea Tanga kwa mchezo na Tabora Utd utakaopigwa ljumaa (Sptemba 29) kwenye Uwanja wa Mkwakwani wakisaka ushindi wa kwanza baada ya kulala 2-1 kwa Dodoma na sare ya 1-l na Mtibwa Sugar.
Fikiri amesema licha ya ugumu uliopo mbele yao, wapinzani wao wasitarajie mchezo mwepesi huku akidai mwanzo mbaya umechangiwa na kucheza michezo mitatu mfululizo ugenini.
Tunaenda kucheza na timu nzuri yenye wachezaji bora, lakini hilo kwetu halitufanyi kuwaogopa kwa sababu timu kama Simba SC imekuwa kipimo kizuri cha kufanyia kazi upungufu uliojitokeza” amesema.
Fikiri aliongeza licha ya kumkosa Haji Ugando aliyepewa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Simba SC, lakini beki wa kati, Khatibu Kombo anaweza kuwepo kwa sababu ameanza mazoezi.