Uongozi wa klabu ya Simba umesema hautakuwa na haraka kufanya mazungumzo ya kuongeza mkataba wa beki wake wa kulia Hassan Ramadhan ‘Kessy’ aliyebakiza miezi sita kumaliza mkataba wa kuichezea timu hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema bado kuna muda mrefu wa kufanya mazungumzo na mchezaji huyo hivyo haoni haraka ya kutaka kumchanganya wakati timu yao kwasasa ipo katika maandalizi muhimu kujiandaa na mechi za ligi zinazotarajia kuendelea Jumamosi ya Desemba 12.

Poppe amesema wanachokifanya kwasasa ni kutoa nafasi kwa mchezaji huyo kufanya maamuzi sahihi ya kuchagua timu anayoipenda ili aweze kuichezea kipindi kijacho.

Balaa: Wanafunzi wa Vyuo Wasafiri Hadi Mlimani City 'Kutumia Vyoo Tu'!
Petr Cech Anena Baada Ya Ushindi Dhidi Ya Olympiakos