Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira  na Walemavu Jenista Mhagama ameipongeza Bank ya Finca kwa kupunguza gharama za ukopaji kwa wananchi, pia amezitaka sekta nyingine za kifedha zinazohusika na utoaji wa mikopo nchini kutenga utoaji wa mikopo kwa wajasiriamali wa wadogo, kati na wakubwa ili kuleta unafuu wa masharti ya ukopaji.

Mhagama amesema hayo alipokuwa akifunga siku ya mwisho ya mafunzo hayo Agosti 27 katika kilele cha mafunzo ya wiki ya huduma ya kifedha na uwekezaji.

Mhagama amesema kuwa mkopo ndiyo kikwazo hususani kwa wajasiriamali wanaoenda kukopa wanashindwa na masharti yakiwemo uwekaji wa hati ya nyumba kama dhamana na riba kubwa.

Mhagama – “Tanzania kuna takribani wajasiriamali milioni tano, ila wengi wao wanashindwa kupiga hatua kutokana na masharti mazito ya mikopo, mfano mama anauza vitumbua unamwamabia alete hati ya nyumba na wakati kapanga chumba kimoja”.

Hivyo, Waziri Mhagama amewataka wadau wote wa maendeleo na banki kukutana ili kujadili ni namna gani wanavyoweza kupunguza masharti kwa wajasiriamali wadogo ili kuwakomboa na kupunguza tatizo la ajira na umasikini nchini.

Afisa Mahusiano na Meneja Masoko wa Banki ya Finca, Spacio Aboubakar amesema walijitahidi kufatilia vikwazo vyote vinavyowakwamisha wajasiriamali na kuvifanyia kazi na kwa sasa kuna unafuu mkubwa wa masharti kwa mkopaji na ulipaji wa riba. Banki ya Finca imekuwa mkombozi kwa wajasiriamali nchini katika maonyesho hayo walifanikiwa kusajili zaidi ya wajasiriamali 4000 wapya.

Katika mafunzo hayo wajasiriamali kutoka vikundi mbalimbali vilishiriki ikiwemo Vikoba pia washindi walikabidhiwa fedha taslimu laki tano ili kuwapa motisha wajasiriamali wengine kushiriki miaka inayofata.

Maonyesho hayo yalikuwa ya tano na huwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta za banki, bima na uwekezaji kutoa elimu kwa wajasiriamali zaidi ya 20,000 na muitikio mkubwa ulikuwa wa wamama kuliko vijana na wanaume

MTV VMAs: Drake afunguka jukwaani ‘anavyomzimia’ Rihanna
Kiwiko Champonza Sergio Aguero, Kujadiliwa Na Kamati Ya Nidhamu