Mshambuliaji kutoka nchini Burundi na klabu ya Young Africans Fiston Abdoul Razack ameanza mazungumzo na klabu tatu tofauti ambazo zimeonyesha nia ya kuhitaji saini yake.

Fiston ameanza kufanya mazungumzo na klabu hizo ambazo bado zinafanywa siri, kufuatia mkataba wake na klabu ya Young Africans kutarajiwa kufikia kikomo mwishoni mwa msim huu. Mkataba wake umesaliwa na miezi miwili kabla ya kumalizika.

Sababu kubwa ya mshambuliaji huyo kuoneshwa mlango wa kutokea, ni kushindwa kufikia kiwango cha kuisaidia klabu hiyo, ambayo ilikua imejiwekea malengo ya kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu 2020/21.

 “Kila mtu anaweza kuwa anajiuliza je, nimeongezewa mkataba au hatima yangu itakuwaje bila kutaka kujua je, ikinibidi kuongeza mkataba nipo tayari kubaki?”

“Nipo kwenye mazungumzo na klabu zaidi ya tatu na tukifikia makubaliano mtazijua.” Amesema Fiston.

Fiston ambaye amewahi kucheza soka nchini Misri, ameshaifungia Young Africans mabao mawili, moja akifunga kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Polisi Tanzania, na lingine alifunga kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Ken Gold.

TAMISEMI kutumia Trilioni 7.6 mwaka wa fedha 2021/2022
Rais Samia kulihutubia Bunge kwa mara ya kwanza