Meneja wa mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich Hansi Flick ana matumaini ya kumtumia mshambuliaji wake kutoka nchini Poland Robert Lewandowski kwenye mchezo wa Ligi Kuu (Bundesliga) mwishoni mwa juma hili dhidi ya Union Berlin.

Flick ameonesha kuwa na matumaini ya kumtumia mshambuliaji huyo hatari, baada ya kukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Lokomotiv Moscow, Jana Jumatano.

Lewandowski ambaye yupo kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa FIFA 2020, alimaliza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya RB Leipzig mwishoni mwa juma lililopita akiwa anachechemea, hali iliyomfanya kukosa mchezo wa jana.

Meneja Flick alisema anaaamini mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32, atakua sehemu ya kikosi chake mwishoni mwa juma hili baada ya kuthibitishiwa anaendelea vizuri.

“Madaktari wamenithibitishia atakua vizuri kwenye mchezo wetu wa ligi mwishoni mwa juma, hakujisikia vizuri baada ya kumaliza dhidi ya RP Leipzig. Ninatarajia Robert Lewandowski atakuwa sawa kwa asilimia 100 Jumamosi.” Alisema meneja huyo wa mabingwa wa Ujerumani, baada ya kuulizwa kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Lewandowski anaongoza katika orodha ya wafungaji katika Bundesliga akiwa maecheza michezo tisa na kutikisa nyavu mara 12 wakati akiwa ameanza katika michezo nane.

FC Bayern Munich hawajafungwa katika michezo yao 17 iliyopita kwenye michuano yote wanayoshiriki.

Katika hatua nyingine meneja Flick amekisifia kikosi chake kwa kucheza soka safi kwenye mchezo wa jana dhidi ya Lokomotiv Moscow, hali iliyoendelea kuthibitisha ubora wao kwenye michuano hiyo kama mabingwa watetezi.

 “Mwaka huu, 2020, umekuwa ya kushangaza kwetu katika Ligi ya Mabingwa, na mafanikio makubwa katika msimu huu.

FC Bayern Munich imefuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo kwa kuongoza msimamo wa kundi A, wakifikisha alama 16, wakifuatiwa na Atletico Madrid wenye alama 9 na Red Bull Salzburg wenye alama 4 na Lokomotiv Moscow wanaburuza mkia wa kundi hilo kwa kupata alama 3.

Paolo Rossi amfuata Diego Maradona
Namungo FC: Tumepata barua ya FIFA