Mzunguuko wa 20 wa ligi kuu ya soka Tanzania bara unataraji kuanza rasmi kesho kwa mchezo mmoja utakaowakutanisha Simba ya Dar es Salaam dhidi ya Stand United ya Shinyanga.
Mchezo huo utaanza kuunguruma mishale ya saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar es Salaam.
Mwamuzi wa katikati atakuwa ni Florentina Zabron kutokea Dodoma, Mwamuzi Msaidizi namba moja atakuwa Ferdinand Chacha wa Mwanza.
Vilevile Mwamuzi msaidizi namba mbili ni Mashaka Mandemwa kutoka Mwanza, Mwamuzi wa akiba ni Gelmina Simon wa Dar es Salaam na Kamishna wa mechi anatoka Arusha, Peter Temu.