Raisi wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez wametoa hofu mashabiki wa klabu hiyo kwa kueleza wazi juu ya mustakabali wa mshambuliaji kutoka nchini Ureno Cristiano Ronaldo.

Perez, amelazimika kulivalia njuga suala la mshambuliaji huyo, kutokana na kuzungumzwa katika vyombo vya habari kila kukicha kuhusu muelekeo wa maisha yake klabuni hapo, ambapo miongoni mwa taarifa za hivi karibuni zilidai yu njiani kuondoka.

Kiongozi huyo amesema, Ronaldo hana mpango wa kuondoka klabuni hapo na wao kama viongozi hawajawahi kufikiria kumuuza kwenye klabu nyingine yoyote zaidi ya kuamini bado huduma yake inahitajika Estadio Santiago Bernabeu.

Ronaldo amekua akitajwa katika harakati za kutaka kusajiliwa na klabu bingwa nchini Ufaransa, Paris-Saint Germain pamoja na klabu ya Man Utd ambayo ilikubalia kumuuza mwaka 2009, kwa ada ya paund million 80.

“Cristiano Ronaldo ni mchezaji bora duniani kwa sasa na ataendelea kuwa kiigizo chema katika klabu hii,” amesema Perez.

“Ni kawaida kwa baadhi ya vyombo vya habari kuzungumza taarifa za uzushi kwa mchezaji mkubwa kwa Ronaldo na nina imani kauli yangu itakua imezima fununu zinazoendelea kuzungumzwa kila kukicha.” Aliongeza kiongozi huyo.

Ronaldo amekua na maisha mazuri katika klabu ya Real Madrid, tangu aliposajiliwa klabuni hapo na mpaka sasa ameshacheza michezo 221 na kufunga mabao 241.

TFF Yamfariji Abdul Mingange Wa Mbeya City
Raphael Kiongera: Kwa Sasa Ninamuachia Mungu