Rais wa klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid Florentino Perez, amethibitisha kuanza mazungumzo na uongozi wa klabu ya Corinthians ya Brazil, kwa ajili ya kufanikisha azma ya usajili wa kiungo Pedro Victor Delmino da Silva (Pedrinho).
Kwa mujibu wa gazeti la The Marca la Hispania, Florentino Perez tayari ameshakutana na kiongozi mkuu wa Corinthians Andres Sanchez, na kufanya mazungmzo ya awali kuhusu usajili wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20.
Sanchez alikua mjini Madrid mwishoni mwa juma lililpita kwa ajili ya kumtembelea mchezaji wa zamani wa Corinthians Ronaldo Di Lima, ambaye kwa sasa ni mmiliki wa klabu ya Real Valladolid.
Katika harakati za matembezi ya kiongozi huyo, ndipo alipokutana na rais wa Real Madrid na inadaiwa walizungumza uwezekano wa kumsajiliwa kwa Pedrinho itakapofika mwezi Januari.
Hata hivyo Sanchez amemtaka kiongozi huyo wa Real Madrid kufanya utaratibu wa kuanza mazungumzo rasmi kuhusu dili hilo, na kama wataafikiana huenda Pedrinho akaanza kuonekana Estadio Santiago Bernabeu msimu huu.
Mpaka sasa tahamani ya Pedrinho haijawekwa wazi, lakini inatarajiwa kufahamika mara baada ya mazungumzo rasmi yatakayofanywa na viongozi wapande hizo mbili.
Pedrinho ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja katika eneo la kiungo, jambo ambalo linatajwa kuwa kivutio kikubwa kwa viongozi wa Real Madrid wakiongozwa na Florentino Perez.