Bingwa wa dunia Floyd Mayweather ameendelea kuonyesha vibweka vya matanuzi ya pesa alizochuma kwa kupanda ulingoni na kuwachakaza wapinzani tangu mwaka 1996 alipoanza kupambana.

Mayweather kama ilivyo ada ameachia picha kwenye mitandao ya kijamii kwa kuoneysha ni vipi anavyojua kutanua kutumia pesa zake.

Picha ya kwanza aliyotuma mtandaoni ilimuonyesha akiwa na rafiki yake mwanamuziki Justin Bieber wakihesabu pesa zilizokua zimefungwa katika maburungutu zaidi ya mawili.

Na baadae walionekana ufukweni akiwa raha huku akipiga misosi ya haja.

Bondia huyo amekuwa na tabia ya kufanya mbwembwe hali ambayo iliwahi kusababisha watu kumuambia kuchangia watu masikini wa Afrika, naye akasema fedha ni zake, hakuna aliyemsaidia kutafuta.

Nyota Ya Jaha Huenda Ikawakia Jangwani 2015-16
Harakati Za Kuelekea Urusi Mwaka 2018