Klabu ya Real Madrid imeendelea kutesa katika nafasi za juu kupitia orodha ya klabu za michezo tajiri duniani ambayo hutolewa kila mwaka na jarida la Forbes la nchini Marekani.

Madrid wameendelea kuwa katika nafasi nzuri katika orodha hiyo kwa mara ya tatu mfululizo, hatua ambayo inaendelea kuuaminisha ulimwengu kwamba uongozi wa The Galacticos umekua na mikakati mizuri ya kusaka fedha kwa faida.

Katika orodha ambayo imetolewa na Forbes usiku wa kuamkia hii leo, Real Madrid imeonyesha ipo katika nafasi ya kwanza kwa kuwa na utajiri wa dola billion 3.26 ambao ni sawa na paund billion 2.08, wakifuatiwa na klabu ya American Football ya Dallas Cowboys pamoja na klabu ya Baseball New York Yankees ambapo kina moja inathamani ya dola billion 3.20 ambazo ni sawa na Paund billion 2.04.

Klabu ya Manchester United imeporomoka katika viwango hivyo vya utajiri duniani ikitokea nafasi ya tatu hadi ya tano kwa kuwa na dola billion 3.10 sawa na pound billion 1.98, huku mahasimu wao Man city wakiwa katika nafasi ya 29 kwa kuwa na billion 1.39 sawa na million 890.

Chelsea wapo katika nafasi ya 31 kwa kumiliki utajiri wa dola billion 1.37 sawa na paund million 877 na Arsenal wanashika nafasi ya 36 kwa utajiri wa dola billion 1.31 sawa na Paund million 839.

FC Barcelona wapo katika nafasi ya nne kwa kuwa na dola billion 3.16 sawa na paund billion 2.02.

Mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich wameshindwa kutinga katika nafasi kumi za juu baada ya kujikuta wakiangukia kwenye nafasi ya 11 kwa kuwa thamani ya dola billion 2.35.

Timu ya Ferrari imekuwa katika nafasi ya 32 kwa kuwa na thmani ya utajiri wa dola billion 1.35 sawa na Paund million 865 ikiwa ni timu pekee kutoka barani Ulaya iliyoingia katika orodha hiyo tofauti na mchezo wa soka.

Klabu za ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani Los Angeles Lakers pamoja na New York Knicks, klabu za American Football New England Patriots na Washington Redskins, klabu ya baseball Los Angeles Dodgers ni miongoni mwa klabu za michezo zilizo kamata nafasi kumi za juu.

Jarida la Forbes limekua likifanya kazi ya kutoa orodha ya thmani ya utajiri wa klabu za michezo pamoja na sekta nyingine duniani tangu mwaka 1998, na hutoa viwango vya thamani ya fedha zinazomilikiwa na klabu hizo kwa dola ya kimarekani.

AY Alivyombadili T.I.D Kutoka Kurap Hadi Kuimba, "Alikuwa hataki Kabisa Kuimba"
Juventus Yazipiku FC Barcelona, Real Madrid Tuzo Za UEFA