Kutajwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwenye jarida maarufu la Forbes Nchini Marekani kama mwanamke mwenye nguvu zaidi duniani kati ya wanawake 100 walioorozeshwa imeleta faida kubwa kwa Tanzania na kufungua fursa zaidi.

Akizungumza na Dar24Media katika kipindi cha mahojia mchambuzi wa masuala ya kisiasa kitaifa na kimataifa Saidi Miraji amesema kuwa kutajwa kwa Rais Samia pia kutamsaidia kupata mialiko mingi zaidi na mataifa mashuhuri, kwasababu mataifa yanapenda kuwatumia watu wenye ushawishi kama alivyo Rais Samia.

Ameongeza kuwa fursa zitakazomjenga Rais Samia zitaleta ushawishi mwingine wa ndani ya Tanzania kutamani alipofikia Rais Samia kitu ambacho kitakuwa chachu ya maendeleo.

Watu 53 wafariki kwa ajali
Ali kiba amkataa Diamond mbele ya waandishi ''Sijui Dini yake"