Hatimaye Shirikisho la Soka Nchini Ureno ‘FPF’ limethibitisha kuvunja mkataba na Kocha Fernando Manuel Fernandes da Costa Santos kwa makubaliano ya pamoja.

Santos mwenye umri wa miaka 68, alishindwa kuiongoza Ureno kufuzu hatua ya Nusu Fainali baada ya kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Morocco huku wengi wakikosoa uamuzi wake wa kumuweka Benchi Nahodha na Mshambuliaji Cristiano Ronaldo.

Santos amekuwa kocha mwenye mafanikio kwenye kikosi cha timu ya Ureno akiisaidia kutwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 2016 sambamba na UEFA Nations League mwaka 2019.

Santos ndiye kocha wa kwanza kuiongoza Ureno kutwaa taji kwenye michuano mikubwa ya Kimataifa, akifanya hivyo katika Fainali za Mataifa ya Ulaya ‘EURO 2016’.

Pia ametwaa ubingwa wa Ligi ya Mataifa ya Ulaya (UEFA Nations League) msimu wa 2018/19.

Kocha Santos alianza kukinoa kikosi cha Urano mwaka 2014 na ameshiriki Fainali Tatu za Kombe la Dunia (2014, 2018 na 2022).

Katika Fainali za Mataifa ya Ulaya, Santos ameiongoza Ureno katika Fainali Mbili (2016 na 2020), na amelingoza taifa hilo mara Tatu katika Michuano ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya (UEFA Nations League).

TFF: Dirisha Dogo la usajili lipo wazi
Ugonjwa wa ajabu waisumbua Ufaransa