Kiungo Gerson Fraga amewapa habari njema Mashabiki na Wanachama wa Simba SC kuwa amepona majeraha yake ya muda mrefu, na muda sio mrefu atarejea uwanjani.

Kungo huyo kutoka nchini Brazil ametuma ujumbe huo kwa Mashabiki na Wanachama wa Simba SC, kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, jana Jumanne (April 13).

Suala kubwa alilolionesha kwenye ujumbe huo, ni kutamani kurejea nchini Tanzania ili akamilishe ndoto za kuitumikia Simba SC, ambayo ililazimika kusitisha mkataba wake, kufuatia majeraha yaliyomkabili kwa muda mrefu.

Fraga ameandika: “Muda wa kurudi uwanjani unakaribia. Namshukuru kila mmoja kwa sapoti. Mkata umeme nitarudi haraka haraka. Nakuja,”

 Wakati Fraga akiweka wazi nia ya kurejea Simba, mmoja wa viongozi wa timu hiyo amesema itategemea na mahitaji ya benchi la ufundi chini ya kocha Didier Gomes Da Rosa.

Kuondoka kwa Fraga Simba SC, kulitoa nafasi kwa uongozi wa klabu hiyo kumsajili kiungo kutoka nchini Uganda, Tadeo Lwanga ambaye amekua kipenzi cha Mashabiki na Wanachama, kufuatia uwezo na umakini anaouonesha kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Tarimba: Young Africans fuateni nyayo za Simba
GSM: Manji anakaribishwa Young Africans

Comments

comments