Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Franco Pablo Martin amesema wachezaji wake walicheza hovyo dhidi ya Geita Gold FC jana Jumatano (Desemba Mosi).

Simba SC ilikua mwenyeji wa mchezo huo wa Mzunguuko wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kocha Franco amesema hakufurahishwa na mwenendo wa kikosi chake kwenye mchezo huo hasa kipindi cha pili, hivyo kuna jambo la kujifunza kwa wachezaji wake katika michezo inayofuata.

Amesema kikosi chake kilishindwa kumliki mpira kama alivyotoa maelekezo, jambo ambalo liliwapa wakati mgumu wa kuwakabili vilivyo wapinzani wao kutoka mkoani Geita.

“Siwezi kufurahishwa na kiwango cha leo (Jana). Nadhani tulicheza mchezo mbovu sana. Hatukumiliki mchezo, hatukuonyesha jitihada.”

“Hatukuonyesha ubora tunaopaswa kuwa nao katika mchezo huu, hasa tena tukiwa nyumbani. Tunahitaji kutawala mchezo lakini kwa kweli mpinzani alitawala sehemu kubwa ya mchezo.”

“Hata tulipopata fursa na nafasi ya kumaliza mchezo hatukufanya hivyo. Tuliwaruhusu kuingia kwenye mchezo baada ya kufunga bao letu la pili. Mwishowe tulipata tabu hadi mwisho. Ikiwa tutacheza hivi, nadhani tutateseka Zambia, na itakuwa vigumu sana kutimiza malengo tuliyonayo.” amesema kocha huyo kutoka nchini Hispania

Mchezo huo ulimalizika kwa Simba SC kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, ambao unaendelea kuwaweka katika nafasi ya pili kwenye Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22.

Awanywesha watoto sumu kisa maisha magumu
WHO yatoa onyo