Meneja wa muda wa Kikosi cha Chelsea, Frank Lampard ameikosoa timu yake kutopambana na kusema kwamba inabidi abadilishe hali hiyo haraka kabla ya mchezo ujao dhidi ya Real Madrid utakaopigwa Jumanne (April 18).
Lampard ametoa kauli hiyo baada ya kupoteza kwa mabao 2-1 katika Ligi Kuu England dhidi ya Brighton & Hove Albion mwishoni mwa juma lililopita.
Amesema Wachezaji wake walikuwa wakionesha kushindwa kutimiza mambo ya msingi. “Inasikitisha kwa kila kilichoonekana kwa upande wetu,”
“Timu bora ilishinda na ingeweza kushinda kwa zaidi. Walicheza kama timu. Wanafanya kazi pamoja kwa muda mrefu.”
“Lakini haitoshi kwa mtazamo wetu. Sehemu zote za msingi za soka kupigana, kukimbia, na mambo hayo tulikuwa na upungufu. Inabidi tujichambue kwa haraka sana.”
“Tuna mchezo mkubwa kesho Jumanne. Hakuna haja ya kuwa chini sana, lakini kitaalamu tunapaswa kuelewa ni kwa nini mamabo yalienda jinsi ilivyokuwa. Na haikuwa nzuri kwetu.”
Chelsea wamepoteza michezo yote mitatu tangu Frank Lampard arejee kama Meneja wa muda wa kikosi.