Meneja wa klabu ya Chelsea Frank Lampard ana mpango wa kukiongezea nguvu kikosi chake, huku wachezaji Jadon Sancho wa Borussia Dortmund na Philippe Coutinho anaecheza FC Bayern Munich kwa mkopo akitokea FC Barcelona wakitajwa.

Lampard anataka kufanya maboresho kwenye kikosi chake baada ya kushindwa kufanya hivyo msimu huu, japo amekamilisha mpango wa kumnasa mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Morocco na klabu ya Ajax Amsterdam, Hakim Ziyech ambaye ataanza kuonekana akiwa na uzi wa Bluu msimu ujao.

Kiungo huyo wa zamani wa The Blues kwa sasa ataendelea kubaki na wachezaji wake makinda wakati msimu wa Ligi Kuu England utakapoendelea, lakini mara utakapokwisha tu na dirisha la usajili kufunguliwa ataanza kukamilisha mpango wake.

Hata hivyo huenda Lamperd akapata upinzani wa kumpata Sancho, kufuatia kiungo kuwa kwenye rada za Mashetani Wekundi (Manchester United), ambao wanaonekana kuongoza kwenye mbio za kumsajili Mwingereza huyo.

Kwa upande wa Coutinho, pia kuna upinzani mkali kutokana na Arsenal kuonekana kuhitaji huduma yake pia.

Sura nyingine mpya anazozisaka Lampard ni beki wa kushoto wa Leicester City, Ben Chilwell, ambaye anaweza kumgharimu Pauni milioni 60, kiungo mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, Kai Havertz na mshambuliaji wa RB Leipzig, Timo Werner.

Kwa upande wa mlinda mlango, meneja huyo anamuwania Roman Burki wa Borussia Dortmund, kutokana na kipa Kepa Arrizabalaga kuwa kwenye mashaka makubwa huko Stamford Bridge.

Ripoti: Kilichotokea baada ya Trump kutishia kutumia jeshi kuzima maandamano
Aristica Cioaba kuanza kazi rasmi