Bosi wa Klabu ya Eintracht Frankfurt ya Ujerumani Markus Krosche, amefunguka kuwa hawana mawasiliano na Mabingwa wa Soka nchini humo FC Bayern Munich kuhusu dili la usajiliwa wa Mshambuliaji kutoka Ufaransa Randal Kolo Muani.

Kolo Muani amekuwa akihusishwa na Klabu kadhaa za Barani Ulaya kutokana na kuwa na msimu bora tangu alipoonesha uwezo mkubwa wakati wa Fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

FC Bayern Munich wamekuwa wakitajwa kuwa na mpango wa kumsajili nyota huyo, kama sehemu ya mipango yao ya kuboresha kikosi chao kuanzia msimu ujao wa Ligi ya Ujerumani na Barani Ulaya.

Klabu nyingine zinazotajwa kumuwania Mshambuliaji huyo ni Mabingwa wa Ufaransa Paris Saint Germain, Manchester United na Chelsea zote za England.

Hivi karibuni ilielezwa kuwa, Bayern wameanza mazungumzo na Frankfurt kwa ajili ya dili la Mshambuliaji huyo, lakini Mkurugenzi Krosche amekanusha.

“Hatuna mawasiliano na FC Bayern Munich kwa ajili ya Kolo Muani, lakini ni kawaida kwa klabu kama Bayern kuwa na mpango na mchezaji mzuri kama huyu.”

“Lakini yeye anajisikia vizuri kuwa hapa, naweza kusema Bayern sio timu pekee inayomuhitaji, zipo timu nyingi zinamuangalia, amesema mkurugenzi huyo.

Clatous Chama aunguruma Morocco
Nasredinne Nabi: Hatujafuzu Nusu Fainali