VINARA wa Ligi Daraja la Kwanza katika kundi (A) klabu ya Friends Rangers, imesajili wachezaji wanne ambao ni Emanuel Gabriel, Fred Cosmas, Mussa John ‘Rooney’ na Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi hiyo unaotarajia kuanza hivi karibuni.

Ofisa Habari wa klabu hiyo Asha Kigundula, alisema kuwa katika kuhimalisha kikosi chao, wameamua
waongeze wachezaji wanne ambao watasaidia kupandisha timu yao.

Kigundula alisema kuwa hata hivyo kikosi chao kitaenda kuweka kambi ya wiki moja Lushoto mkoani Tanga, kama sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili.

Alisema kuwepo kwa wachezaji hao ambao waliwahi kuvituzimikia klabu kubwa hapa nchini kutasaidia kujenga zaidi kikosi chao ambacho kimekuwa moto wa kuotea mbali.

Alisema katika msafara huo jumla ya watu 40, wataenda katika kambi hiyo maalum, kikiongozwa na Katibu Mkuu wa timu hiyo na Heyry Chibakasa (HerryMzozo).

Rangers yenye maskani yake magomeni Kagera Dar es Salaam, ndiyo wanaoshika usukani wa Ligi Daraja la kwanza katika kundi A.

Simba Yaiongeza Nguvu Kwenye Safu Ya Ulinzi
Safari Za Barani Afrika Kumtimua Ronaldo Mjini Madrid