Mchezaji Jeando Fuchs aliyekua sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa kilichotwaa ubingwa wa Ulaya chini ya umri wa miaka 19 mwaka 2016, amejilipua na kukubali kurejea nchini Cameroon.
Fuchs ambaye ni mzaliwa wa nchini Cameroon, amechukua maamuzi ya kurejea nyumbani, baada ya kuona kuna umuhimu wa kuitumikia timu ya taifa ya asili yake, huku akibebwa na sheria za shirikisho la soka duniani FIFA kwa kuchukua maamuzi hayo.
Mpaka anaamua kurejea nyumbani, Fuchs alikua hajaitwa wala kuitumikia timu ya taifa ya wakubwa ya Ufaransa.
Tayari kocha mkuu wa timu ya taifa ya Cameroon Clarence Clyde Seedorf, amemuita kwenye kikosi kitakacho ingia kambini kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika 2019 dhidi ya Morocco, na baadae mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Brazil itakayochezwa mwezi huu.
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 21, kwa sasa anaitumikia klabu ya Sochaux inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Ufaransa (Ligue 2).
Fuchs ambaye ni kiungo mkabaji, alicheza sambamba na mshambuliaji Kylian Mbappe katika kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 19 cha Ufaransa, pia alishiriki kwenye fainali za kombe la dunia kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 mwaka 2017.
Kocha Seedorf pia amemuitwa kikosini kwa mara ya kwanza baada ya miaka minne kupitia mchezaji mwenye asili ya Tunisia, Jean-Armel Kana-Biyik.
Kwa mara ya mwisho beki huyo mwenye umri wa miaka 29, ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani Andre Kana-Biyik, aliitumikia Cameroon katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Ureno walioibuka na ushindi wa mabao matano kwa moja, Februari 2014.
Kikosi kilichotajwa kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika dhidi ya Morocco na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Brazil.
Makipa: Andre Onana (Ajax Amsterdam, Netherlands), Idriss Carlos Kameni (Fenerbahce, Turkey) na Fabrice Ondoa (Oostende, Belgium)
Mabeki: Fai Collins (Standard Liege, Belgium), Michael Ngadeu Ngadjui (Slavia Prague, Czech Republic), Oyongo Bitolo (Montpellier, France), Yaya Banana (Panionos, Greece), Jerome Onguene (Red Bull Salzburg, Austria), Gaëtan Bong (Brighton, England), Jean-Armel Kana-Biyick (Kayserispor, Turkey) na Jeando Fuchs (Sochaux, France)
Viungo: Zambo Anguissa (Fulham, England), Georges Mandjeck (Maccabi Haiffa, Israel), Pierre Kunde Malong (Mainz, Germany), Arnaud Djoum (Hearts, Scotland) na Petrus Boumal (FK Ural, Russia)
Washambuliaji: Jacques Zoua (Astra Giurgiu, Romania), Fabrice Olinga (Royal Excel Mouscron, Belgium), Eric-Maxim Choupo-Moting (PSG, France), Toko Ekambi (Villarreal, Spain), Clinton Njie (Marseille, France), Stephane Bahoken (Angers, France) na Christian Bassogog (Henan Jianye, China)