Mabingwa wa soka nchini Uingereza, Chelsea huenda wakakubali kumrejesha beki wa kushoto kutoka nchini Brazil, Filipe Luis, mjini Madrid baada ya kushindwa kumtumia ipasavyo msimu uliopita.

Kwa mujibu wa taarifa zilizofanyiwa uchunguzi na kituo cha televisheni cha Sky Sports, zinaelezwa kwamba Luis amekuwa na wakati mgumu wa kutimiziwa maazimio yaliyopo kwenye mkataba wake ya kuchezeshwa katika kikosi cha kwanza tangu alipoelekea magharibi mwa jiji la London msimu uliopita akitokea kwenye klabu ya Atletico Madrid.

Tayari imeelezwa kwamba Atletico Madrid wapo mbioni kutoa kiasi cha paund milioni 15 kama ada ya usajili wa beki huyo mwenye umri wa miaka 29, huku mshahara wake kwa juma ukitarajia kuwa paund elfu 80.

Mazingira ya kucheza katika kikosi cha kwanza kila juma kwa mchezaji huyo, yamekua magumu kutokana na meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho, kumtumia mara kwa mara beki wa kushoto kutoka nchini Hispania Cesar Azpilicueta.

Tangu alipojiunga na klabu ya Chelsea July 16 mwaka 2014, Filipe Luis ameitumikia The Blues katika michezo 15.

Van Gaal Alikuwa Na Nia Ya Kuipasua Bayern Munich.!
Fahamu Vibweka Vya Aliyemrushia Noti Bandia Sepp Blatter