Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman amesema Zanzibar ina fursa na rasilimali nyingi za kiuchumi za kuwawezesha vijana kujiajiri kwa kufanya kazi wanazoziweza, ili kuondokana na tatizo la umasikini.

Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameyasema hayo huko Jadida Wete Pemba alipozungunza na wananchi na wapenzi wa chama hicho katika mfululizo wa Mikutano ya hadhara inayoendelea.

Amesema, kinachohitajika ni kuwatengenezea mazingira ili vijana hao waweze kujiajira na kuajirika katika fani na sekta mbali mbali za kiuchumi zikwemo mahotelini biashara na kilimo ili kuweza kufidia mahitaji ya soko na kuondoa changamoto ya umasikini.

Aidha ameongeza kuwa Zanzibar pia inavipaji vingi kwa ufundi ambapo vijana wanahitaji kuwezesha ili kutumia zana za kisasa zitakazowawezesha kuzalisha bidhaa bora katika matumizi ya viwandani na majumbani na kuongeza mapato yao na kuenuka kiuchumi.

Nyaraka za siri: Trump kupandishwa kizimbani Miami
George Mpole: Nasubiri kwa hamu 2023/24