Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba, ameweka wazi kuwa kuna fursa pana katika soko la korosho kutokana na nchi nyingi duniani kuhitaji korosho zilizobanguliwa.

Mgumba amesema hayo akiwa kwenye mkutano na viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia zao la korosho ambapo amesema kwa sasa Tanzania ina masoko mawili ya korosho ambayo ni India na Vietnam, lakini kuna fursa pana ya soko la korosho katika nchi za kiarabu, Ulaya,Marekani, China.

Ameongeza kuwa uongezwaji wa thamani ya korosho umekuwa wa kiasi cha chini sana huku akizitaja faida zitokanazo na uongezwaji thamani wa zao hilo nchini kabla ya kusafirisha nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kuongeza ajira na kupata bei nzuri ya korosho.

“Uongezwaji wa thamani wa zao la korosho pamoja na bidhaa zingine zitokanazo na korosho una faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuongeza ajira kupata bei nzuri ya korosho kupanua wigo wa kodi kuinua uchumi wa nchi na kupata soko la uhakika wa korosho zinazozalishwa hapa nchini”. amesema Mgumba.

RC Dar: Wasimamizi elimu acheni wizi
Kenya: Jaji mkuu amtaka rais kulivunja Bunge