Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemuahidi Rais wa Misri Abdel Fatah Al-Sisi kutua ujumbe wa walimu wa Kiswahili nchini Misri kama kuunga mkono jitihada za nchi hiyo kufundisha Lugha ya Kiswahili katika Vyuo vya Elimu ya juu nchini Misri kama lugha ya kimkakati.
Rais Samia ameyasema hayo leo alipofanya mkutano na waandishi wa habari wa nchini humo akiwa na Rais Al Sisi mara baada ya kuwasili nchini Misri.
Aidha Rais Samia amempongeza Rais Al-Sisi kwa jitihada hizo akisema ni njia nzuri ya kujipanga kimkakati.
Katika hatua nyingine ya mazungumzo hayo marais hao wamezungumzia ushirikiano wa pamoja katika nyanja za Ulinzi, elimu, nishati na ushirikiano wa Kijeshi.
Pia Rais Samia amemtaka Rais Al-Sisi kuhakikisha vikwazo vyote vinavyoendelea katika mradi wa Umeme wa Mwalimu Nyerere vinaondolewa ili kukamilisha mradi huo mapema.
Rais Samia Suluhu Hassan amefika Leo nchinj Misri kwa Ziara ya siku 3.