Mpango wa usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Brazil na klabu ya Santos, Gabriel Barbosa Almeida (Gabigol), huenda ukawauwia vigumu viongozi wa klabu Juventus FC ambao tayari wameshapiga hatua ya mazungumzo ya uhamisho.

Juventus, tayari wameshakubaliwa kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 19, kwa ada ya uhamisho ya Euro milion 20, lakini mpaka sasa hawajafanya mzungumzo binafsi na Gabigol.

Jambo hilo limeonyesha kumuumiza kichwa rais wa klabu ya Santos, Modesto Roma ambaye ameonyesha kuwa tayari kufanya biashara ya kumuuza mshambuliaji huyo katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

Kiongozi huyo amesema, wanajitahidi kusaidia suala la mazungumzo baina ya Juventus na Gabigol likamilishwe kwa wakati.

“Tumeshatuma barua kwa Wagner (wakala wa Gabigol), Valdemir na Lindalva (wazazi wa Gabigol) ili kusaidia jambo hili,”

“Kama wataona inafaa kufanya mzungumzo na mchezaji ili akamilishe mpango wa kwenda kucheza soka nchini Italia, itakua ni vizuri.” Alisema Modesto Roma

Hata hivyo imeanza kuhisiwa utata wa jambo hilo, unasababishwa na uwepo wa ofa nyingine kutoka kwenye klabu ya Barcelona ya nchini Hispania ambayo imeonyesha nia ya kumuhitaji Gabigol.

Video: Msanii ajipiga risasi mdomoni na kupost video Facebook akitafuta ‘Kiki’
Mustakabali Wa Roberto Mancini Kufahamika Leo