Beki wa kati kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia Ya Kongo Gabriel Zakuani, ametangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya nchi hiyo, akiwa na umri wa miaka 32.

Beki huyo wa klabu ya Gillingham, amefikia maamuzi ya kustaafu kuitumikia timu ya taifa, baada ya kucheza michezo 30 tangu mwezi Januari mwaka 2013.

“Ahsante kwa The Leopard, nimekua mchezaji wa timu hii kwa kipindi cha miaka mitano, ninaamini nimefanikisha mpango nilioukusudia wa kuwa mtetezi wa taifa langu katika michuano ya kimataifa. ” Zakuani aliviambia vyombo vya habari.

“Bado ninaipenda timu hii, nitaendelea kuithamini na kuifuatilia kila itakapokua inacheza ndani na nje ya Kongo. Ninawatakia kila la kheri wachezaji waliobakia kwenye timu huu, hususan vijana ambao wanabeba jukumu la kuitetea Kongo kimataifa.”

Zakuani alikua sehemu ya kikosi cha Jamuhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo kilichoshiriki fainali za Afrika mwaka 2015 na kuamliza katika nafasi ya tatu, pia alijumuishwa kwenye kikosi hicho wakati wa fainali za Afrika za mwaka 2013 na 2017.

Wakati Zakuani akichukua maamuzi hayo, gwiji wa soka wa Jamuhuri Ya Kidemokrasia ya Kongo Lomana LuaLua, amemtumia salamu za pongezi na shukurani, kwa kutangaza maamuzi hayo magumu.

“Ninamshukuru sana Zakuani kwa kufanya maamuzi haya magumu, itatoa nafasi kwa vijana chipukizi kuchukua nafasi yake kwenye kikosi cha timu yetu ya taifa,”  Alisema Lualua ambaye aliwahi kutamba kwenye ligi ya England akiwa na klabu za Newcastle Utd na Portsmouth.

Mwezi Mei mwaka 2017, Zakuani alishindwa kufikia makubaliano na viongozi wa klabu ya Northampton Town inayoshiriki ligi ya Ufaransa.

Alianza maisha yake ya soka la kulipwa barani Ulaya akiwa na klabu ya Leyton Orient na kisha Peterborough zote za England.

Pia amewahi kucheza soka akiwa na klabu za Fulham na Stoke City (England), na baadaye alitimkia Ugiriki kujiunga na klabu ya Kalloni.

Zlatan Ibrahimovic afunga bao la 500
Breaking News: Waitara atetea Ubunge wake, atangazwa kuwa mshindi Ukonga