Wakala wa Kiungo kutoka nchini Ufaransa Paul Pogba, Gad Cohen amesema kiungo huyo anatakiwa kukaza buti kama anataka kujiunga na Ligi Kuu Saudi Arabia maarufu ‘Saudi Pro League’.

Kwa mujibu wa ripoti, Pogba alizungumza na mabosi wa Al-Ittihad kwenye usajili wa dirisha la kiangazi kwa mujibu wa ripoti.

Cohen, ambaye amehusika na madili makubwa kutoka Saudi Arabia alizungumza kupitia TMW akidai Pogba alikuwa na nia ya kutimkia huko.

“Kweli Pogba alionyesha nia. Sidhani kama jambo baya, anaweza kuwa miongoni mastaa wakubwa kwenye ligi hiyo, lakini anatakiwa kuimarika zaidi ili kuleta ushawishi. Anatakiwa kukaza Juventus, aonyeshe dunia yeye ni mchezaji wa aina gani,” alisema wakala huyo.

Taarifa za hivi karibuni zimeripoti kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa aliumia baada ya ushindi wa mabao 2-0 katika mechi ya Serie A kabla ya mechi za kimataifa.

Pogba aliingia kipindi cha pili katika kuendelea baada ya kupata majeraha, huku kocha wa Juventus, Max Allegri akisisitiza bado hawakupewa taarifa kuhusu ukubwa wa jeraha lenyewe.

Maswali yaliibuka kuhusu afya ya kiungo huyo kutokana na majeraha kumuandama mara kwa mara ambayo yameletea changamoto.

Mwenendo wa Pogba umeendelea kuwa jambo la dharura ambalo Juventus inapaswa kulishughulikia kwa tahadhari na uangalifu mkubwa.

Tetemeko Morocco: Idadi ya vifo yafikia Watu 2900
Niyonzima aipeleka Young Africans Makundi CAF