Mwezi sasa na zaidi umekatika tangu sauti ya Mtangazaji wa Kipindi cha Jahazi kinachorushwa Clouds Fm Gadner G Habash aliyekuwa mume wa lady jaydee ilivyosikika  akisema “Na sina neno na yule mtoto wa kike. Nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi”

Kauli hii ilipokelewa  kwa hisia tofauti mpaka kupelekea Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hamis Kigwangallapamoja na  mwanasheria wa mwimbaji huyo kumuandikia barua mtangazaji huyo ya kuomba radhi kwa udhalilishajii aliofanya kwa mteja wake lakini bado kukawa na ukimya.

Wiki hii Bongo5 ilifanya mahojiano na Gardner ‘Captain’ ambapo alisema amesema anaheshimu faragha ya muimbaji huyo ambaye pia aliwahi kuwa mkewe kwa miaka isiyopungua 15.

“Kusema kweli sitaki kulizungumzia suala la Lady Jaydee, naheshimu faragha yake,” alisema Gadner. “Ile issue ilikuzwa na mitandao ya kijamii, na mitandao ya kijamii inajua kutengeneza mambo hata yasiyokuwepo,”

Mtangazaji huyo amesema hana tatizo na mwanadada huyo kwa kuwa kila mtu alishasonga mbele na anaendelea na mambo yake.

Uvumi unaosambaa ni kwamba wimbo wa Ndi ndi ndi unaelezea maisha yao waliyokuwa wakiishi wanandoa hao hivyo kudaiwa kwamba ameimbiwa Mtangazaji huyo.

 

Serikali Kukusanya Bilioni 200 Kiwanda cha Nondo
Medeama SC Wabadili Mbinu Za Kuwasili