Uongozi wa Klabu ya Geita Gold uko kwenye mazungumzo na Kocha Mkuu wa KMKM, Hemed Suleiman ‘Morocco’ kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho.

Hatua hiyo inajiri baada ya Geita kuachana na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Fredy Felix ‘Minziro’ baada ya mkataba wake kuisha tangu Mei 28 mwaka huu.

Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo zinasema, Morocco ndiye aliyependekezwa kuchukua nafasi ya Minziro kwa ajili ya msimu ujao.

“Seleman (Matola) alikuwa ni chaguo la kwanza ila baada ya kuona mambo hayaendi vizuri viongozi wakahamishia nguvu kwa Morocco ambaye hakutakuwa na shida kubwa sana kwenye kufikia muafaka suala la masilahi binafsi,” kilisema chanzo hicho.

Akizungumzia hilo Mwenyekiti wa Geita, Leonard Bugomola amesema wapo makocha wengi waliotuma wasifu wao (CV) na mchakato wa kupitia jina moja baada ya lingine unaendelea ingawa suala la nani atachaguliwa hilo litafahamika hivi karibuni.

Kocha Hemed Suleyman Morocco

Kwa upande wa Morocco alipotafutwa na alisema yeye hajui lolote linaloendelea ingawa anasikia tu kuhusu jambo hilo.

“Nimesikia kama ambavyo nawewe umesikia ila siwezi kusema ni kweli au laah! muda utakapofika kila kitu nadhani kitakuwa wazi,” amesema

Zaha azigonganisha tatu kwa pamoja
Warabu kuharibu dili zito Old Trafford