Aliyekuwa mgombea urais wa CHADEMA 2015, Edward Lowassa ambaye alikihama Chama Cha Mapinduzi ameweka wazi taarifa za kutaka kurudi CCM, ambapo amesema kuwa hana mpango na wala hafikirii kufanya jambo hilo.

Ameyasema hayo kufuatia kauli iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kuwa Lowassa ana mpango wa kurudi katika chama hicho kama baadhi ya wananchama wengine wa CHADEMA walivyofanya.

“Ni jambo la jabu sana, nataka kumwambia Mrisho Gambo aache uongo sina mpango wa kurudi CCM na siihitaji CCM, wananchi wapuuze maneno hayo, ni uongo, anastahili kuchukuliwa adhabu, nasikitika sana, anataka kuchukua wajibu ambao sio wake, haihitaji kuwa msemaji wangu na wala simuhitaji kuwa msemaji wangu,”amesema Lowassa

Aidha, amesema kuwa kitendo cha mkuu wa mkoa wa Arusha kusema hadharani kwamba Lowassa amemuomba amkutanishe na Rais Magufuli kwani anataka kurudi kwenye chama, ni kitendo kisichofaa kwa kiongozi mkubwa kama yeye, na kumtaka aache mara moja kwani yeye sio msemaji wake.

Hata hivyo, hivi karibuni Gambo alisikika akisema kuwa amefuatwa na baadhi ya watu ambao wametumwa na Lowassa, kumuomba amsaidie kukutana na Rais Magufuli ili aweze kurejea CCM, kwani uamuzi ambao aliufanya mwaka 2015 wa kuhama chama ulikuwa ni uamuzi wa hasira.

 

Video: Kinara wa michango kumtibu Lissu huyu, CCM haikamatiki
Magazeti ya Tanzania leo Novemba 27, 2017