Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo ametoa hoja akitaka bunge liahirishe shughuli zake ili wabunge wajadili kuhusu upandaji wa bei za bidhaa nchini.

Mbunge huyo amesema hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan aliagiza wabunge kuwapa elimu sahihi wananchi wao kuhusu upandaji wa bei za bidhaa muhimu hivyo akaomba bunge lipewe nafasi ya kujadili kwa kina jambo hilo.

Naye Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson amesema ni kweli kuna tatizo hilo katika maeneo mengi nchini ambapo bidhaa zinazowahusu wananchi wa kawaida zimepanda kwa kiasi kikubwa.

Dkt. Tulia amesema hoja ya mbunge huyo hajaridhishwa nayo kwa namna ilivyo kwa kutumia kanuni ya 54 (4) kwamba inampa nafasi ya kuagiza kitu gani kifanyike.

“Kutokana na hilo, nakuagiza Kaimu kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni (Dk Dotto Biteko) kwamba jambo hili mlitazame na kufuata utaratibu ambao huwa unatumika katika kusaidia inapotokea bei zinakuwa juu,” ameagiza Spika.

Kwa siku za hivi karibuni bidhaa zimepanda zaidi katika maeneo tofauti nchini ambapo wawakilishi wa wananchi bungeni wameanza kulilalamikia ikiwemo mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma wakitaka Serikali kutafuta namna ya kuokoa hali hiyo kwani kazi ya Serikali ni kulinda watu wake.

Mashabiki 60,000 kuishuhudia Simba SC Kwa Mkapa
ASFC: Simba Vs Pamba FC yapigwa kalenda